UZIMA WA MILELE KWA NANI?
Jifunze kuhusu wokovu na injili ya YESU KRISTO.
“Kama vile Baba alivyo na uzima ndani Yake, vivyo hivyo amempa Mwana kuwa na uzima ndani Yake.” (Yoh.5:26).
Uzima wa milele siyo jambo la muda! Kana kwamba, eti, utaishi kwa milele na milele, mwaka hadi mwaka hadi mwaka! Baba na Mwana tu wanao huo Uzima ndani Yao! Uzima wa milele ni jambo la hali, jambo la tabia!
Uzima (wa milele) ni hali au tabia ya Mungu Mwenyewe! Uzima wa milele ni Utakatifu, Upendo, Wema, Huruma, Uvumilivu, Ufadhili, Nuru. Mungu anaweza kulifanya jiwe lidumu hata milele. Bado hiyo haimaanishi kwamba lile jiwe linao uzima wa milele! Ni vivyo hivyo kwetu!
“Huu ndio ushuhuda, ya kwamba, Mungu ametupa uzima wa milele, nao huo uzima umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao uzima, yeye asiye na Mwana hana uzima.” (1 Yoh.5:11,12).
Unaona? Uzima wa milele ni ndani ya Yesu! Unakumbuka Yesu alisema, ‘Mimi ni njia, na kweli na uzima.’ (Yoh.14:6). Yeye Mwenyewe ni Uzima! Hamna uzima, hamna uzima wa milile nje ya maisha na tabia ya Yesu Kristo. Haitoshi kuamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. “Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka.” (Yak.2:19). Lazima ninaye Yesu Kristo ndani yangu. Maisha Yake ndani yangu huo ndio ni uzima wa milele ndani yangu! “Yeye aliye naye Mwana, anao uzima, yeye asiye na Mwana hana uzima.” Uzima wa milele ni hali ya tabia ya Mungu, kwa hiyo Mungu hakuweza kutupa Uzima wa Milele bila kutupa Uzima Wake, bila kutupa Roho Yake. Kwa hiyo Petro anatufundisha,
“Kwa kuwa uweza Wake WA UUNGU umetukirimia vitu vyote vipasavyo UZIMA NA UTAUWA… Kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa WASHIRIKA WA TABIA YA UUNGU…”. (2 Petro 1:3,4).
Na tena katika Waebrania,
“…hao (baba zetu) kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali Yeye (Mungu Baba) kwa faida yetu, ILI TUUSHIRIKI UTAKATIFU wake.” (12:10).
Yohana anatutangaza kwa wazi ukweli huu mkuu, “Watoto wadogo, ninyi MMETOKANA NA MUNGU, nanyi mmewashinda kwa sababu YEYE ALIYE NDANI YENU ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu.” (1 Yoh.4:4).

